DHANA JUU YA HISTORIA
by Ahmedi Mnungano Allah amuhifadhi
Historia kama somo ina sehemu kubwa sana ya kuchangia katika maendeleo ya mwanadamu.
Ni kutokana na historia binaadamu wa leo hufahamu vipi watu waliotangulia walifanikiwa au walifeli katika maisha yao. Na hivyo kujifunza juu ya namna ya kuyakabili mazingira yake.
Hata hivyo fundisho lolote lipatikanalo kutokana na historia, linategemeana sana na mtizamo wa muhusika juu ya historia.
Ipo mitzamo mikuu miwili:
(i) Mtizamo wa Kiislamu na
(ii) Mtizamo wa Kikafiri.
Kabla hatujaendelea na lengo letu la kuangalia historia katika Uislamu, ni vyema tuone makafiri wanasema nini juu ya historia
(i) Mtizamo wa Kikafiri Juu ya Historia na Udhaifu Wake
Historia kwa waandishi wengi wa kileo hufasiriwa kama ni kumbukumbu ya matendo ya mwanadamu. Matendo hayo yawe ni yenye kumwezesha mwanadamu kupata mahitaji yake muhimu kutoka kwenye maumbile ya asili (nature).
Kwa makafiri mahitaji muhimu ya wanadamu ni chakula, nguo na makazi.
Kwa hiyo matendo yote ya mwanadamu yana lengo moja tu; la kumpatia mahitaji muhimu ya maisha ambayo ni chakula, nguo na makazi. Kwa mtizamo wao huo makafiri wameyahusisha matendo yote ya mwanadamu na uzalishaji vitu au uzalishaji mali (Material Production).
Kwa hiyo basi wakawa wanaiangalia historia katika ngazi mbili.
Katika ngazi ya kwanza huiangalia historia kama somo lenye kuelezea mapambano ya mwanadamu dhidi ya mazingira yake. Mapambano ambayo ni ya lazima ili mwanadamu aweze kupiga hatua katika maendeleo.
Katika ngazi ya pili, makafiri huitazama historia kama somo lenye kuonyesha vipi harakati za uzalishaji mali zinavyoathiri uhusiano baina ya mtu na mtu.
Hii ni kutokana na imani yao kuwa mwanadamu ni mnyama kama wanyama wengine. Na badiliko lolote litakalotokea kwa binadamu aonekane tofauti na wanyama wengine, basi litakuwa ni zao la harakati zake dhidi ya maumbile (Nature).
Kwa hiyo kwa makafiri kusoma historia ni muhimu kwa sababu huwasaidia kuelewa mabadiliko ya mahusiano kati ya mtu na mazingira yake na kati ya mtu na mtu.
Na kwa njia hiyo wanaweza kufahamu hali ya mwanadamu iliyopita na ya sasa na hivyokuweza kujiandaa ili kuukabili vyema wakati ujao.
Mtizamo huu wa makafiri katika kuiainisha historia una udhaifu mkubwa sana. Wao wamemtazama mwanaadamu na mazingira yake au kwa maneno mengine viumbe na mazingira yao na kumwachilia mbali Muumbaji wa vyote hivyo viwili.
Mtizamo wa Makafiri Juu ya Chanzo cha Dunia,Mwanaadamu na Lengo la Uhai Wake.
Baada ya kuona mtizamo wa kikafiri juu ya historia, itakuwa ni vyema tuone wanasema nini juu ya chanzo cha dunia, mwanaadamu na lengo la uhai wake. Katika kukiendea kipengele hiki tutaangalia hoja za wanafalsafa wa kisoshalist au wakomunist. Kisha tutaangalia wanasayansi wanavyosema. Hii itatusaidia kufahamu endapo ukafiri (ukanaji kuwepo kwa Mola Muumba) ni zao la maendeleo ya sayansi au la.
Makafiri hudai vile vile kuwa binadamu ni zao la kiumbe dhalili chenye chembe hai moja tu (Unicellular creature) ambacho kilibadilika kutoka katika hali hiyo ya uduni kupitia hatua ya kuwa pweza, chura, mjusi, nyani hadi kuwa mtu kamili.
Kwa hivyo kwa makafiri binaadamu ni zao la mabadiliko ya kidogo kidogo (evolutionary changes) na kwamba hakuumbwa na Allah(s.w).
Kwani tangu hapo kwa Mtazamo wao Allah(s.w) hayupo (wana’uudhubillah).
Jitihada kubwa sana zimefanyika kuzieneza fikra hizi na zimepewa umuhimu mkubwa katika somo la Historia mashuleni. Tukiangalia kitabu cha historia cha shule za sekondari kidato cha kwanza, kilichotolewa na Taasisi ya Elimu – Tanzania ukurasa wa 11 kuna maelezo yafuatayo juu ya chanzo cha mwanadamu:
Origin of Man:
“Man came into existence together with other animals more than thirty million years ago.
In the beginning, man belonged to the family of primates which include apes, monkeys, and gorillas.
These primates lived in troops in trees.
As well as walking on all fours, these primates had developed different uses for their limbs. The fore-limbs were used for catching and gripping.
Hind-limbs were used for standing on branches or on the ground. As the forests became smaller some of these primates had to live in open grasslands.
The new environment and experience forced this primate to adopt to life in the grasslands.
Over time his hind-limbs became specialized for walking and standing.
For example, he had to stand up, watch out for enemies and run away from them.
This freed the fore-limbs which could now be used for tool using.
He used sticks to dig-up roots or turn-over stones in the search for insects.
Using tools and bi-pedalism were accompanied by the development of the brain.
These three were very crucial changes in the evolution of man, who began to appear different from other animals.
However man is distinguished from the other primates by his ability to design tools for specific purposes.
At first the body of man’s ancestors was closer to that of chimpanzee in appearance.
It was huge and covered with plenty of hair. Gradually as he developed by improving his methods of obtaining food, shelter, and clothing his shape became that of a modern man. By about 50,000 years ago true man had appeared.
This process is known as evolution.”
Huo ndio mtizamo wa makafiri juu ya chanzo cha mwanadamu. Mtizamo ambao kila kukicha hupandikizwa kwenye vichwa vya kizazi kichanga katika somo la Historia mashuleni.
Chimbuko la Mtizamo wa Makafiri Juu ya Chanzo cha Dunia na Mwanadamu.
Labda itakuwa vyema kabla ya kuchambua mtizamo huu wa makafiri huu wa kumkana muumba juu ya chanzo cha dunia na mwanadamu, tuangalie kwanza chimbuko la mtizamo wenyewe.
Karl Marx, mwanzilishi wa itikadi ya kijamaa hutambulika katika karne ya ishirini kuwa ndiye chimbuko la ukafiri huu wa kumkana muumba(atheism).
Hatumaanishi hapa kuwa kabla ya Karl Marx hawakuwepo makafiri, la.
Bali tunamtaja yeye kwa vile ndiye aliyechukua jitihada kubwa kuusomesha na kuueneza ukafiri huu katika zama zetu hizi.
Ukafiri ulioshadidi katika nchi zilizokuwa zikijiita za kikomunisti ni zao la kazi ya Karl Marx.
Kwa fikra zake Marx, na wafuasi wake, ulimwengu huu hauna muumba na kwamba ulimwengu huu huongozwa na kanuni za kibaiolojia, kikemia na kifizikia.
Na hivyo basi sayansi ndio jawabu la kila kitu.
Kutokana na dhana hii Karl Marx na wafuasi wake hukana kuwepo kwa Allah(s.w) kwa hoja kwamba imani juu ya Allah(s.w) ni imani ya kibubusa na kwamba kumkana Allah(s.w) ni suala la kisayansi.
Chimbuko la Fikra za Karl Marx Kwa vile Juzuu yetu hii inaangalia suala zima la historia, itakuwa vyema tuonyeshe kwa muhtasari chimbuko la fikra za Marx.
Kuibuka kwa fikra za Marx na makafiri wengine juu ya chanzo cha dunia na suala la kuwepo Mungu Muumba kwa ujumla, kumechochewa na hali ya kutisha iliyoondoa mahusiano yote kati ya Dini na maisha huko Ulaya, hatimaye kutenganisha itikadi ya Dini na utaratibu wa maisha ya kijamii.
Hali hiyo ilitokeaje?
Kwanza, Kanisa lilihodhi peke yake haki ya kuielewa na kuifafanua Biblia kwa kumkataza mtu yeyote nje ya makada wao kujaribu kuielewa na kuifahamu Biblia.
Halafu kukafuatia kuingiza katika mafundisho ya Dini hiyo imani za kibubusa (dogmas) ambazo zilikuwa hazieleweki, hazikubaliki na wala haziaminiki.
Kanisa likazifanya imani hizo zisizoeleweka “mafumbo ya Mungu” au “ibada”.
Mfano dhahiri ni imani ya kibubusa juu ya Ekaristi (Chakula cha jioni cha Bwana) imani ambayo ilipingwa na Martin Luther, John Calvin na Ulrich Swingli na kuanzisha madhehebu ya Waprotestanti.
Suala la Ekaristi ni uzushi usio na msingi wowote katika kitabu kitakatifu, katika historia ya Wakristo wa mwanzo na hata katika mabaraza ya Kanisa.
Kilichotokea ni kwamba kwa mila zao Wakristo walikuwa wakila mkate na kunywa mvinyo wakati wa pasaka na wakakiita chakula cha jioni cha Bwana.
Hatimaye Kanisa likadai kuwa mkate na mvinyo vilibadilika kuwa mwili na damu ya Yesu.
Yeyote atakayekula mkate na mvinyo wakati wa kuingia katika Dini hiyo atapata Rehma kwa kupitia mwili na damu ya Yesu.
Kanisa likashinikiza dai hili kwa wafuasi wake na likakataza mijadala ya hoja kwa tishio la kutengwa.
Zaidi ya imani hizi potofu zilizoingizwa katika Dini hiyo zilizoandamana na kuwakataza watu kuzithibitisha katika Biblia (ambayo walizuiliwa kuifafanua), Kanisa likajiingiza katika kutoa nadharia juu ya uhai na ulimwengu.
Likaziunga mkono nadharia fulani fulani za kijiografia, kihistoria na kifizikia zilizokuwa maarufu wakati huo, nadharia ambazo zilijaa makosa na udhanifu wa ajabu na Kanisa likadai kuwa nadharia hizo hazihojiki, hazisahihishiki, hazipingiki na hazibadilishiki.
Hili lilikuwa pigo la mwisho kwani imani hizo zisizokuwa za kisayansi zilikuwa zimejengwa juu ya uwongo, na hivyo rahisi kutenguliwa kwa majaribio mepesi tu.
Zaidi ya hayo kutafuta na kuthibitisha elimu ni jambo ambalo Mwenyezi Mungu ameusia akili ya binaadamu kudadisi kwa makini upeo wa uwezo wake bila Mwenyezi Mungu kutanguliza tafsiri maalum.
Juu ya hilo, A. Nadwi anaelezea kwa ufasaha kama ifuatavyo juu ya matokeo ya msiba huu mkuu katika kitabu chake mashuhuri, “What the World Lost by Muslim Decadence”.
“Moja ya makosa makubwa yaliyotendwa na mapadri wa Kizungu, na pengine laweza kuwa kosa kubwa kabisa lililofanywa dhidi ya Dini ni kwamba waliingiza katika vitabu vyao vitakatifu baadhi ya elimu za kibinaadamu na habari za zama zao juu ya historia, geografia na sayansi ya maumbile.
Habari hizo za sayansi zilizoingizwa wakati huo zilionekana sahihi kabisa na ikadhaniwa kuwa ni kweli zisizo shaka na zisizoweza kutangulika”.
“Hata hivyo, kilele cha elimu katika kipindi fulani si kauli ya mwisho na elimu haituami, kwani elimu ya binadaamu daima huongezeka na hukua.
Lau Dini itajengwa juu ya elimu ya binadaamu, basi jengo hilo limesimama katika mchanga unaodidimia.
Yawezekana kuwa mapadri walipandikiza katika vitabu vyao habari hizo kwa nia njema kabisa.
Lakini wamejidhuru wenyewe na Dini yao, kwani mapandikizi hayo yalianzisha mapambano yasiyofaa kati ya sayansi, hoja na ‘Dini’, na hatimaye ‘Dini’ ilishindwa vibaya sana.
Ilikuwa ni Dini ambayo kweli na urongo na haki na batili vimechanganywa na hivyo watetezi wake wasingeweza kupata chochote isipokuwa kushindwa ambako hawakuweza tena kurudisha hadhi yao. Kibaya zaidi ni matoekeo yake; kwani Ulaya yote ilipuuza au karibu kuikana kabisa Dini”.
“Zaidi ya hayo, mapadri waliyainua tena yote yaliyoelezwa na yalikuwa yakijulikana na kila mtu pamoja na sehemu ya ufafanuzi wa Agano la Kale na Jipya kuhusu jiografia na sayansi ya maumbile.
Wakazipa habari hizi “utukufu wa kidini” na wakazifanya kuwa ni sehemu ya Dini na hivyo kila mtu lazima aamini na akikatae kilicho kinyume na habari hizo.
Wakaandika vitabu juu yake na wakauita udhanifu huo wa jiografia ‘Jiografia ya Kikristo’ na wakaishikilia kwa jino na ukucha na kila asiyeamini udhanifu huo akaitwa mpagani”.
“Yote hayo yalitokea katika kipindi ambacho hoja ilikuwa ikiibuka huko Ulaya na wanasayansi walikuwa wakianza kuvivunja vizingiti vya ‘Dini’, na kuikosoa jiografia ya Kikristo waziwazi pamoja na vitabu vyake vingine wakatangaza kutoamini kwao fikra hizo kuwa ni takatifu na wakaonesha ugunduzi wao kupitia majaribio yao.
Hili likaamsha ghadhabu ya Kanisa na viongozi wao huko Ulaya wakawahesabu wanasayansi hao kuwa ni wapotofu na makafiri.
Hivyo wakaimwaga damu yao na wakawanyang’anya mali zao kwa madai kuwa wanautetea Ukristo, na zikaanzishwa Mahakama za Uchunguzi ili kuwaadhibu wale ambao kwa maneno ya papa ‘wale makafiri na waasi waliotawanyika katika miji, nyumba, misitu, mapango na mashamba’.
Mahakama za Uchunguzi hazikupoteza muda na zikafanya kazi kwa mori na zikajitahidi zilivyoweza kumteketeza kila adui katika ulimwengu wa Kikristo. Wakaanzisha taasisi za wapelelezi katika nchi zote, wakichunguza kila mtu kwa msisitizo ambao ulimfanya mwanatheolojia mmoja wa Kikristo aseme, “hakuna mtu awezaye kuwa Mkristo na kufa katika hali ya kawaida”.
“Inahisiwa kuwa walioangamizwa na mahakama hizi walifika elfu mia tatu, na kati ya hao elfu thelathini na mbili walichomwa moto wakiwa hai.
Miongoni mwao alikuwepo mwanafizikia mashuhuri Bruno ambaye fikra zake juu ya uwingi wa ulimwengu zilighadhibisha kanisa kiasi ambacho walimwua bila kumwaga tone la damu.
Hii ilikuwa na maana ya kumchoma moto akiwa hai! Alikuwepo pia mwanasayansi maarufu Galileo aliyeamini kuwa dunia inalizunguka jua na imani yake ilimgharimu uhai wake”.
“Mambo yalipofikia hatu hii, wasomi na wagunduzi walishindwa kuvumilia na wakatangaza uasi wao dhidi ya Kanisa, mapadri na dhidi ya wote wanaoshikilia ukale.
Wakakipinga kila kilichohusiana nao iwe imani au elimu, sayansi au maadili.
Wakajenga uadui kwanza na dini ya Kikristo, halafu na dini zote bila kubagua; na mapambano kati ya wanasayansi na hoja dhidi ya viongozi wa Dini ya Kikristo yakawa ni mapambano kati ya sayansi na dini kwa ujumla.
Wanamapinduzi wakahitimisha kuwa sayansi na Dini havipikiki chungu kimoja.
Mtu ilimpasa achague moja na asuse jingine. Dini kwao ilileta kumbukizi za damu za mashahidi waliopoteza maisha yao kwa ajili ya sayansi na utafiti na kumbukizi za watu wasio na hatia waliouliwa kwa sababu ya ukatili wa mapadri na kwa sababu ya kutoamini kwao. Katika akili zao Dini ilileta taswira ya nyuso zilizosawajika, zenye ukali na mapaji ya uso yenye makunyazi, ghadhabu isiyo na subira na ujinga usio kiasi.
Walichukizwa katika nyoyo zao na wakaamua kuchukia na kupigana dhidi ya Kanisa na kila walilowakilisha au walilohubiri.
Vizazi vilivyofuata vilirithi hisia na kumbukizi hizi chungu”.
Marx alikuwa miongoni mwa wanafalsafa walioathiriwa na hali hiyo. Lakini kosa walilofanya ni kule kushindwa kutofautisha Dini na wale waliohodhi uongozi wa Dini.
Kwa vile Ukiristo (dini) huo kule Ulaya ndio ulikuwa ukiongoza mafundisho juu ya kuwepo kwa Mungu Muumba na kwa vile chuki ilishamea dhidi ya dini, Marx na wenzake walijitoa kwenye dini na hivyo kujitoa kwenye imani juu ya kuwepo kwa Mungu Muum
No comments:
Post a Comment