UKUMBUSHO-TAREKHE

 UTANGULIZI

By ahmed mnungamo

Shukurani zote njema zinamstahiki Allah(s.w) aliye Bwana na Mlezi wa walimwengu wote. Rehema na Amani ziwaendee Mitume wake wote pamoja na wale wanaofuata mwenendo wao katika kuhuisha Uislamu katika jamii.

Lengo  la  kuumbwa  watu  na  kuletwa  hapa  ulimwenguni  ni kumuabudu  Mola  wao,  Allah  (s.w),  kama  inavyobainishwa  katika Qur-an:

وَمَا خَلَقْتُ الْجِنَّ وَالْإِنْسَ إِلَّا لِيَعْبُدُون



"Sikuwaumba  majini  na  watu  ila  wapate  kuniabudu".    (51:56)

 Kumuabudu  Allah  (s.w)  kama  lengo  la  maisha  ni  kumtii  Allah (s.w)  kwa  unyenyekevu  katika  kila  kipengele  na  kila  nukta  ya maisha  ya  mtu  akiwa  binafsi  na  akiwa  katika  jamii.

Ili watu  waweze  kumuabudu  Mola  wao  katika  kila kipengele  na  kila  nukta  ya  maisha  yao,  hawanabudi  kwanza,  kuwa waumini  wa  kweli  wa  Allah  (s.w)  na  kisha  kufanya  juhudi  za makusudi  za  kuwa  makhalifa wa Allah  katika  jamii.  

Makhalifa wa Allah  ni  wale  wanaoiongoza  jamii  kwa  kufuata  mwongozo  wa Allah (s.w)  kupitia  kwa  Mitume  yake  na  vitabu  vyake.    Waumini wakifanya  jitihada  za  kusimamisha  ukhalifa katika  jamii,  Allah (s.w)  ata  wawezesha  kufikia  lengo  la  kuumbwa  kwao  kama anavyoahidi:

وَعَدَ اللَّهُ الَّذِينَ آمَنُوا مِنْكُمْ وَعَمِلُوا الصَّالِحَاتِ لَيَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِي الْأَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِينَ مِنْ قَبْلِهِمْ وَلَيُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِينَهُمُ الَّذِي ارْتَضَىٰ لَهُمْ وَلَيُبَدِّلَنَّهُمْ مِنْ بَعْدِ خَوْفِهِمْ أَمْنًا ۚ يَعْبُدُونَنِي لَا يُشْرِكُونَ بِي شَيْئًا ۚ وَمَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذَٰلِكَ فَأُولَٰئِكَ هُمُ الْفَاسِقُون

"Mwenyezi  Mungu  amewaahidi  wale  walioamini  miongoni mwenu  na  kufanya  vitendo  vizuri,  kuwa  atawafanya  makhalifa katika  ardhi  kama  alivyo  wafanya  makhalifa  wale  waliokuwako kabla  yao,  na  kwa  yakini  atawasimamishia  Dini  yao Aliyowapendelea,  na  atawabadilishia  amani  baada  ya  khofu  yao. Wawe  wananiabudu,  hawanishirikishi  na  chochote.    Na watakaokufuru  baada  ya  hayo,  basi  hao  ndio  wavunjao  amri zetu."    (24:55)

Lengo  la  kuletwa  Mtume  wa  mwisho,  Muhammad(s.a.w),nalo linabainishwa  katika  aya  ifuatayo:

هُوَ الَّذِي أَرْسَلَ رَسُولَهُ بِالْهُدَىٰ وَدِينِ الْحَقِّ لِيُظْهِرَهُ عَلَى الدِّينِ كُلِّهِ وَلَوْ كَرِهَ الْمُشْرِكُون

"Yeye(Allah)  ndiye    aliyemtuma  Mtume  wake(Muhammad)  kwa uongofu  na  kwa  dini  ya  haki  ili  kuifanya  iwe  juu  ya  dini  zote (itawale  katika  jamii)  ijapokuwa  washirikina  watachukia." (9:33,61:9)

Makala  hii imekusudiwa  kuwaonesha  waumini,  kwa kurejea  historia,  uwezekanao  wa  kutekeleza  dhima  hii  kuu  ya kuutawalisha  Uislamu  katika  jamii.  Ili  kuwafikisha  wasomaji kwenye  lengo  tarajiwa,  Makala hii  ya  "Historia ,"  kuanzia  Mtume  Adam(a.s)mpaka  hivi  leo, imewasilisha  maudhui  yake  kwa  anuani  ya  mada  kuu  zifuatazo:

1. Dhana  juu  ya  Historia.

2. Historia  ya  Uislamu  kabla  ya  Muhammad(s.a.w).

3. Historia  ya  Uislamu  wakati  wa  Muhammad(s.a.w).

4. Ungozi  wa  Dola  ya  Kiislamu  wakati  wa  Makhalifa  wa Mtume(s.a.w).

5. Kuhuisha  Uislamu  wakati  wa  Tabiin.

6. Kuhuisha  Uislamu  wakati  wa  Tabiin  Tabiin.

7. Kuhuisha  Uislamu  katika  karne  ya  20  A.D.

8. Historia  ya  kuhuisha  Uislamu  Tanzania.

NB:
Pia katika makala hii tutakazimika kuelezea matukio
mengine ya kihistoria ambayo yataendana na hali na muda kwa kueleza ili liweze kufahamika na kuwafanya wapenzi wasomaji wa page hii kuendana na wakati.

No comments:

Post a Comment