Mwaka Mpya Wa Kiislamu Na Hukumu Ya Kusherehekea

Mwaka Mpya Wa Kiislamu Na Hukumu Ya Kusherehekea

Tunaingia kwenye mwaka mpya wa Kiislam (Hijriyyah). Je, vipi tuukaribishe mwaka huu wetu mpya? Na nini hukumu ya kusherehekea? Na nini umuhimu wa miezi ya Kiislamu?

Kuhesabika Mwaka Mpya 
Miaka yetu ya Kiislam imeanza kuhesabika baada ya Nabiy (Swalla Allahu 'alayhi wa aalihi wa sallam)  na Maswahaba kuhajiri (Hijrah) kutoka Makkah kwenda Madiynah. 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) akatoa ushauri kuwa kwa vile ni mara ya kwanza wanahamia katika mji ambao wataanza kutekeleza shariy’ah ya Kiislam, basi ni bora kuanza kuhesabu ya miaka kwa kuanzia mwezi huo waliohajiri, ambao ulikuwa ni mwezi wa Muharram.

Na pia inasemekana kuwa 'Umar (Radhwiya Allaahu 'anhu) alikuwa akipata barua kutoka kwa magavana wa nchi mbalimbali zilizokuwa chini ya Uislamu, na zilikuwa zikiandikwa majina ya miezi bila tarehe. Akawashauri Maswahaba wenzake kuwa kuweko na tarehe. Wako waliopendekeza tarehe zianze kwa kufuata miaka ya Kirumi, na wako waliopendekeza zianze kwa miaka ya kifursi. Mwishowe wakakubaliana ianze pale alipohamia Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Madiynah.

Na mwaka huu wa Kiislam ambao unafupishwa kama H au Hijriyyah, tarehe 1 Muharram H ilikuwa ni sawa na tarehe 16 Julai 622 M. Na ndivyo hivi inavyohesabika mpaka leo.

Nini Maana Ya Hijrah (Kuhama)
Neno 'hijrah' kwa kiarabu mara nyingi linatarjumiwa kuwa ni 'uhamiaji', lakini haina maana tu ni kuhama nchi kwa nchi au mji kwa mji, au maskani kwa maskani, bali ina maana pia 'kuondoka', 'kusogea', 'kuacha', 'kuepukana', 'kujitenga'.  Na Qur-aan inatuthibitishia hayo; mfano mtu kuihajiri Qur-aan ina maana kuihama Qur-aan:
وَقَالَ الرَّسُولُ يَا رَبِّ إِنَّ قَوْمِي اتَّخَذُوا هَـٰذَا الْقُرْآنَ مَهْجُورًا ﴿٣٠﴾
Na Rasuli akasema: “Rabb wangu! Hakika watu wangu wameifanya hii Qur-aan (kuwa ni) yenye kuhamwa. [Al-Furqaan]

Neno la  مَهْجُورًا  ndio lilokusudiwa kuhajiri. 
Pia:
  فَآمَنَ لَهُ لُوطٌ ۘ وَقَالَ إِنِّي مُهَاجِرٌ إِلَىٰ رَبِّي ۖ إِنَّهُ هُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُ ﴿٢٦﴾
Basi Luwtw akamwamini; na (Ibraahiym) akasema: “Hakika mimi nahajiri kwa ajili ya Rabb wangu; hakika Yeye Ndiye Mwenye enzi ya nguvu Asiyeshindika, Mwenye hikmah wa yote. [Al-‘Ankabuwt: 26]

Hayo ni maneno ya Nabiy Ibraahiym ('Alayhis-Salaam) kutokana na kauli ya Ibn 'Abbaas na Adhw-Dhwahaak. Na kauli nyingine ni maneno ya Nabiy Luutw ('Alayhis-Salaam]. Nabiy Ibraahiym alipoona kwamba watu wake hawataki kumsikiliza na wameshikilia kubakia katika upotofu na kushindwa kwake kuwafanyia da'wah ndipo alipoamua kuhajiri kuelekea Syria. [Tafsiyr Ibn Kathiyr]   
Ufafanuzi wa hijra unapatikana pia katika Hadiyth za Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) pale Maswahaba walipomuuliza:
...أيُّ الْهِجْرَةِ أَفْضَلُ، قَالَ: ((أَنْ تَهْجُرَ مَا كَرِهَ رَبُّكَ))
Hijrah gani iliyokuwa bora zaidi? Akasema: ((Ni kuhama yale Anayochukia Rabb wako)) [Swahiyh An-Nasaaiy 4176]
Na:
 عَنْ عَبْدِ اللَّهِ بْنِ عَمْرٍو (رضي الله عنهما) قَال: قَال رَسُولُ الله صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ: ((الْمُسْلِمُ مَنْ سَلِمَ الْمُسْلِمُونَ مِنْ لِسَانِهِ وَيَدِهِ, وَالْمُهَاجِرُ مَنْ هَجَرَ مَا نَهَى اللَّهُ عَنْهُ)) متفق عليه
Imepokelewa kutoka kwa ‘Abdullaah in ‘Amr (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: “Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Muislamu ni yule anayeweka amani kwa watu (ambaye Waislamu wenziwe wanasalimika) kwa ulimi na mkono wake. Na mhamaji (hijrah) ni yule anayehama Aliyoyakataza Allaah)) [Al-Bukhaariy na Muslim]

Kwa hiyo, kuhama ni dalili ya ‘iymaan kwa kujeipusha na batili na kuelekea kwenye haki, hali ambayo itamuweka Muislamu katika uhusiano mzuri zaidi na Rabb wake. Na hivyo tunaweza kusema kuwa Hijrah inaweza kuwa ni:
  • Hijrah kutoka katika kila aina ya shirk na badala yake kuelekea katika Tawhiyd.
  • Hijrah kutoka katika ujinga na badala yake kuelekea katika nuru ya ‘ilmu.
  • Hijrah ni kutoka katika bid’ah na badala yake kuelekea katika Sunnah.
  • Hijrah kutoka katika faragha ya mambo ya upuuzi na badala yake kuutumia wakati kwa ajili ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa)  
  • Hijrah kutoka katika madhambi, upotofu na badala yake kuelekea katika twaa’ah (utiifu) ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa).
  • Hijrah katika kujeipusha na kila kitendo kitakachosababisha kumuingiza mtu motoni na badala yake kufanya ‘amali zinazopelekea kupata Jannah.  
Hijrah inamjenga Muislam kuwa ni 'Mujaahid' (mwenye kufanya jihaad) kwa ‘iymaan yake, na ndio maana tunaona katika Qur-aan Aayah nyingi zinataja ‘iymaan, hijrah na jihaad pamoja.
 إِنَّ الَّذِينَ آمَنُوا وَالَّذِينَ هَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ أُولَـٰئِكَ يَرْجُونَ رَحْمَتَ اللَّـهِ ۚ وَاللَّـهُ غَفُورٌ رَّحِيمٌ ﴿٢١٨﴾
Hakika wale walioamini na wale waliohajiri na wakapigana jihaad katika njia ya Allaah, hao wanataraji rahmah ya Allaah, na Allaah ni Mwingi wa kughufuria, Mwenye kurehemu. [Al-Baqarah: 218]

وَالَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ وَالَّذِينَ آوَوا وَّنَصَرُوا أُولَـٰئِكَ هُمُ الْمُؤْمِنُونَ حَقًّا ۚ لَّهُم مَّغْفِرَةٌ وَرِزْقٌ كَرِيمٌ﴿٧٤﴾
Na wale walioamini na wakahajiri na wakafanya jihaad katika njia ya Allaah, na wale waliotoa makazi na wakanusuru, hao ndio Waumini wa kweli. Watapata maghfirah na riziki karimu. [Al-Anfaal: 74]

الَّذِينَ آمَنُوا وَهَاجَرُوا وَجَاهَدُوا فِي سَبِيلِ اللَّـهِ بِأَمْوَالِهِمْ وَأَنفُسِهِمْ أَعْظَمُ دَرَجَةً عِندَ اللَّـهِ ۚ وَأُولَـٰئِكَ هُمُ الْفَائِزُونَ﴿٢٠﴾
Wale walioamini na wakahajiri na wakafanya jihaad katika njia ya Allaah kwa mali zao na nafsi zao; wana daraja kuu kwa Allaah. Na hao ndio waliofuzu.

يُبَشِّرُهُمْ رَبُّهُم بِرَحْمَةٍ مِّنْهُ وَرِضْوَانٍ وَجَنَّاتٍ لَّهُمْ فِيهَا نَعِيمٌ مُّقِيمٌ﴿٢١﴾
Rabb wao Anawabashiria kwa rahmah kutoka Kwake na radhi (Zake) na Jannaatwatapata humo neema (za kila aina) zenye kudumu.

خَالِدِينَ فِيهَا أَبَدًا ۚ إِنَّ اللَّـهَ عِندَهُ أَجْرٌ عَظِيمٌ﴿٢٢﴾
Ni wenye kudumu humo abadi. Hakika Allaah Kwake kuna ujira adhimu. [At-Tawbah: 20-22]

Ndugu Waislam, tumekosa fursa ya kufanya Hijrah pamoja na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Maswahaba zake, lakini kuna aina nyingine ya hijrah ambayo itatupatia thawabu maradufu. Nayo ni kuhajiri kutoka katika yote yaliyoharamishwa na kuelekea katika yatakayomridhisha Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa). Maswahaba walimuuliza Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
Kubakia katika twaa’ah (utii) katika zama za fitnah kama zama zetu hivi sasa, thawabu zake ni sawa na kuhajiri na Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kwa dalili:
 عنْ مَعقِلِ بن يسارٍ ، رضي اللَّه عنْهُ ، قَالَ : قال رَسُولُ اللَّهِ صَلّى اللهُ عَلَيْهِ وسَلَّم: ((العِبَادَةُ في الهَرْجِ كهِجْرةٍ إلَيَّ )) رواهُ مُسْلمٌ
Kutoka kwa Ma'qil bin Yasaar (Radhwiya Allaahu 'anhu)  ambaye amesema: Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((‘Ibaadah katika fitnah ni kama Hijrah kuelekea kwangu)) [Muslim]

Ndugu Muislam! Jiepushe na yote Aliyoyakataza Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) na Rasuli Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam). Pia zidisha ‘ibaadah kwa wingi khasa katika miezi hii mitukufu.

Haifai Kusherehekea Mwaka Mpya
Haifai Waislam kusherehekea mwaka mpya wa Kiislam na kupongezana kwa sababu hizo ni mila za kikafiri. Waisalamu wameiga mila zao mfano makafiri wanavyosherehekea Krismasi inayodaiwa kuwa ni tarehe aliyozaliwa Nabiy ‘Iysaa ('Alayhis-Salaam) basi na Waislam wakazua kusherehekea mazazi ya Nabiy (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam).  Kisha wakazua kusherehekea siku za kuzaliwa (birthdays)! Na makafiri waliposherehekea mwaka mpya wa Gregorian, Waislamu wakaanza kusherehekea mwaka mpya wa hijri.

Kusherehekea huko, ni vile baadhi ya Waislamu kutumiana maamkizi katika njia mbali mbali mitandao ya kijamii kwa kuamkiana mfano: 'Hongera za mwaka mpya' (Happy new year) au ‘Kullu ‘Aam wa ‘antum bikhayr’.


Imaam Muhammad bin Swaalih Al-‘Uthaymiyn alipoulizwa je, nini hukumu ya kupeana pongezi kwa mwaka mpya wa Kiislam au kuamkiana na kuombeana du'aa?

Akajibu:
"Ikiwa mtu atakupa pongezi au kukuamkia, basi muitikie lakini usianzishe wewe kufanya hivyo. Na rai iliyo bora kabisa katika mas-alah haya ni kwamba mtu atakapokuambia: 'Pongezi ya mwaka mpya' basi sema: 'Tunamuomba Allaah aufanye uwe mwaka wa kheri na baraka kwako'. Lakini usianzishe abadan wewe kwa sababu sikuona mapokezi yoyote kwamba Salafus-Swaalih (watangu wema) walikuwa wakiamkiana au kupeana hongera katika mwaka mpya wa Hijrah."      

Umuhimu Wa Kutumia Miezi Ya Kiislamu
Ingawa miezi ya mwaka wa Gregorian ndio inayotumika katika shughuli za kiofisi, lakini tunapaswa Waislamu kuthamini pia miezi yetu ya Kiislamu kwa kujitahidi kadiri tuwezavyo kuitumia katika shughuli zetu, maandishi yetu n.k. Miezi ya Kiislamu imekadiriwa na Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) kabla ya kuumbwa mbingu na ardhi kama Anavyosema (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ عِدَّةَ الشُّهُورِ عِندَ اللَّـهِ اثْنَا عَشَرَ شَهْرًا فِي كِتَابِ اللَّـهِ يَوْمَ خَلَقَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضَ مِنْهَا أَرْبَعَةٌ حُرُمٌ ۚ ذَٰلِكَ الدِّينُ الْقَيِّمُ ۚ فَلَا تَظْلِمُوا فِيهِنَّ أَنفُسَكُمْ ۚ وَقَاتِلُوا الْمُشْرِكِينَ كَافَّةً كَمَا يُقَاتِلُونَكُمْ كَافَّةً ۚوَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ مَعَ الْمُتَّقِينَ﴿٣٦﴾
Hakika idadi ya miezi mbele ya Allaah ni kumi na mbili katika hukmu ya makadirio ya Allaah, (tangu) siku Aliyoumba mbingu na ardhi. Kati ya hiyo, (iko miezi) minne mitukufu. Hivyo ndiyo Dini iliyo nyoofu. Basi msijidhulumu humo nafsi zenu (kwa kufanya maasi), na piganeni vita na washirikina wote kama wao wanavyokupigeni vita nyote. Na jueni kwamba Allaah Yu Pamoja na wenye taqwa. [At-Tawbah: 36]

Kuna umuhimu ya kuwafundisha watoto wetu waifahamu miezi ya Kiislamu kwa kuihifadhi yote. Inasikitisha kwamba Waislamu wengi hawaifahamu miezi yao. Ukimuuliza mtoto wa Kiislamu akutajie miezi ya Gregorian atakutajia yote bila ya kukosea, lakini ukimuuliza miezi ya Hijri haijui.

Orodha ya Majina ya miezi ya Kiislamu

1
Muharram
محرّم
2
Swafar
صفر
3
Rabiy’u Al-Awwal
ربيع الاول
4
Rabiy' Al-Aakhir
ربيع الآخر
5
Jumaada Al-Uwlaa
جمادى الأول
6
Jumaada Al-Aakhir
جمادى الآخر  
7
Rajab
رجب
8
Sha’baan
شعبان
9
Ramadhwaan
رمضان
10.
Shawwaal
شوّال  
11.
Dhul-Qa’dah
ذو القعدة
12
Dhul-Hijjah
ذو الحجة

Wa biLLAahit-Tawfiyq

HISTORIA YA UISLAMU KABLA YA MUHAMMAD(S.A.W)

BY Ahmed Mnungamo:

Katika  makala hii  imeelezwa  kwa  muhtasari  historia  ya  mitume  waliotajwa katika  Qur’an  waliomtangulia  Mtume  Muhammad(s.a.w).

Mitume  waliotajwa katika  Qur’an  kabla  ya  Mtume(s.a.w)  ni    hawa  wafuatao:

 (1)  Adam(a.s)
(2)  Idris(a.s)
(3)  Nuhu(a.s)
(4)  Hud(a.s)
(5)  Salih(a.s)
(6)  Ibrahim(a.s) (7)  Lut(a.s)
(8)  Ismail(a.s)
(9)  Is-haq(a.s) (10)Ya’aquub(a.s) (11)  Yusufu(a.s) (12)  Ayyuub(a.s) (13)Shu’ayb(a.s) (14)  Musa(a.s) (15)  Harun(a.s) (16)  Al-yasaa(a.s)
 (17)  Dhul-Kifil(a.s)
 (18)  Daud(a.s)
(19)Sulaiman(a.s) (20)Ilyasa(a.s) (21)  Yunus(a.s) (22)  Zakaria(a.s) (23)  Yahya(a.s) (24)  Isa(a.s)

Lengo  la  kupitia  historia  ya  mitume  hawa  ni  kuwaandaa wasomaji  na  kuwapa  ari  na  hamasa  itakayo  wawezesha  kuhuisha na  kusimamisha  Uislamu  katika  jamii  kama  walivyofanya  mitume hao  na  wafuasi  wao.

 Kuna  mafundisho  mengi  msomaji anayoyapata  kutokana  na  historia  ya  kila  Mtume.

Katika  Makala  hii  pia  imeelezwa  historia  ya  watu  wema  na  watu waovu  waliotajwa  katika  Qur’an  na  mafunzo  yatokanayo  na makundi  haya  mawili.

Watu  wema  waliotajwa  katika  Qur-an  ni

(1)  Vijana  wa  pangoni

(2)  Dhulqarinain 

(3)  Al-Khidhri

(4)  Luqman

Watu  waovu  waliotajwa  katika  Qur-an  ni

(1)  Watu  waliovunja  amri  ya  Jumamosi

(2)  Karun  na  Hamana

(3) Watengenezaji  mahandaki  ya  Moto

(4)  Watu  wa  mji  waliomuua  muislamu  kwa  kusadikisha Mitume  wa  Allah(s.w)

Baada  ya  utangulizi  huu,  tutaanza  kupitia  historia  ya  Mtume baada  ya  Mtume  na  mafunzo  yatokanayo  na  kisha  tutamalizia  kwa kupitia  historia  ya  makundi  ya  watu  wema na  watu  waovu na mafunzo  yatokanayo.

 Ikumbukwe  kuwa  lengo  kuu  la  kupitia  historia  hii  ni  kupata mafunzo  yatakayotuwezesha  kuhuisha  na  kusimamisha  Uislamu katika  jamii.                      
[18:34, 9/10/2017] Ahmed Mnungamo: ADAM(A.S)

Kuumbwa  kwa  Adam(a.s)

Adam(a.s)  ni  mtu  na  Mtume  wa  Allah(s.w)  wa  kwanza.

Adam(a.s)  ameumbwa  kwa  udongo  uliofinyangwa  ukafanywa kuwa  sanamu  la  mtu  kisha  likapuliziwa  roho  na  kuwa  mtu  kamili kama  tunavyofahamishwa  katika  Qur-an:

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِنْ صَلْصَالٍ مِنْ حَمَإٍ مَسْنُون

فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِنْ رُوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِين

Na  (kumbuka)  Mola  wako  alipowaambia  Malaika,  “Hakika  Mimi nitamuumba  mtu  kwa  udongo  mkavu  unaotoa  sauti,  wenye kutokana na matope meusi yaliyovunda.”

“Basi nitakapomkamilisha  na  kumpulizia  roho  inayotokana  na  Mimi, basi  mumuangukie  kwa  kumtii.”      (15:28-29)

إِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي خَالِقٌ بَشَرًا مِنْ طِينٍ

فَإِذَا سَوَّيْتُهُ وَنَفَخْتُ فِيهِ مِنْ رُوحِي فَقَعُوا لَهُ سَاجِدِين

(Kumbuka)  Mola  wako  alipowaambia  Malaika:    Hakika  mimi nitaumbwa  mtu  kwa  udongo.
Na  nitakapomkamilisha  na kumpulizia  roho  inayotokana  na  mimi  basi  msujudieni  (kama ishara  ya  kumheshimu).    (38:71-72).

Hadhi  ya  Adam(a.s)  na  Kizazi  Chake Kabla  ya  Adam(a.s)  kuumbwa,  Allah(s.w)  aliwafahamisha Malaika  kuwa  atamleta  Khalifa  (kiongozi)  katika  ardhi atakayesimamisha  Ufalme  wa  Allah(s.w)  (Dola  ya  kiislamu)  kwa kufuata  mwongozo  wake  Allah(s.w). 

 Mazungumzo  baina  ya Allah(s.w)  na  Malaika  wake  juu  ya  ukhalifa  wa  Adam(a.s)  na  kizazi chake  tunayapata  katika  aya  zifuatazo:

وَإِذْ قَالَ رَبُّكَ لِلْمَلَائِكَةِ إِنِّي جَاعِلٌ فِي الْأَرْضِ خَلِيفَةً ۖ قَالُوا أَتَجْعَلُ فِيهَا مَنْ يُفْسِدُ فِيهَا وَيَسْفِكُ الدِّمَاءَ وَنَحْنُ نُسَبِّحُ بِحَمْدِكَ وَنُقَدِّسُ لَكَ ۖ قَالَ إِنِّي أَعْلَمُ مَا لَا تَعْلَمُونَ
(Wakumbushe  watu  khabari  hii):   Wakati  Mola  wako alipowambia  Malaika:    “Mimi  nitaleta  Khalifa    katika  ardhi.” Wakasema  (Malaika):  “Utaweka  humo  watakaofanya  uharibifu humo  na  kumwaga  damu,  hali  sisi  tunakutukuza  kwa  sifa  zako  na kukutaja  kwa  utakatifu  wako?”  Akasema  (Mwenyezi  Mungu): “Hakika  Mimi  nayajua  msiyoyajua.”(2:30)

وَعَلَّمَ آدَمَ الْأَسْمَاءَ كُلَّهَا ثُمَّ عَرَضَهُمْ عَلَى الْمَلَائِكَةِ فَقَالَ أَنْبِئُونِي بِأَسْمَاءِ هَٰؤُلَاءِ إِنْ كُنْتُمْ صَادِقِين
Na  (Mwenyezi  Mungu)  akamfundisha  Adam  majina  ya  vitu vyote,  kisha  akaviweka  mbele  ya  Malaika,  na  akasema (kuwaambia  Malaika):    “Niambieni  majina  ya  vitu  hivi  ikiwa mnasema  kweli  (kuwa  nyinyi  ndio  wajuzi  wa  mambo).”(2:31)

قَالُوا سُبْحَانَكَ لَا عِلْمَ لَنَا إِلَّا مَا عَلَّمْتَنَا ۖ إِنَّكَ أَنْتَ الْعَلِيمُ الْحَكِيمُ
Wakasema  (Malaika):    “Utakatifu  ni  wako!    Hatuna  ilimu isipokuwa  ile  uliyotufundisha;  bila  shaka  wewe  ndiye  Mjuzi  na ndiye  Mwenye  hikima.”    (2:32).

قَالَ يَا آدَمُ أَنْبِئْهُمْ بِأَسْمَائِهِمْ ۖ فَلَمَّا أَنْبَأَهُمْ بِأَسْمَائِهِمْ قَالَ أَلَمْ أَقُلْ لَكُمْ إِنِّي أَعْلَمُ غَيْبَ السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَأَعْلَمُ مَا تُبْدُونَ وَمَا كُنْتُمْ تَكْتُمُون
Akasema  (Mwenyezi  Mungu):    “Ewe  Adam!    Waambie  majina yake.”    Alipowaambia  majina  yake  alisema  (Mwenyezi  Mungu) “Sikukwambieni  kwamba  mimi  najua  siri  za  mbinguni  na  za ardhi; tena najua  mnayoyadhihirisha  na  mliyokuwa mnayaficha?”.(2:33)

وَإِذْ قُلْنَا لِلْمَلَائِكَةِ اسْجُدُوا لِآدَمَ فَسَجَدُوا إِلَّا إِبْلِيسَ أَبَىٰ وَاسْتَكْبَرَ وَكَانَ مِنَ الْكَافِرِين

Na  (wakumbushe  watu  khabari  hii):    Tulipowaambia  Malaika “Msujudieni  Adam”.  Wakamsujudia  wote  isipokuwa  Iblis;  akakataa na  akajivuna;  na  (tokea  hapo)  alikuwa  katika  makafiri(2:34)

 Kutokana  na  aya  hizi  tunajifunza  yafuatayo:

1.Adam(a.s) nakizazi chake(wanaadamu) wamekusudiwa  kuwa  Makhalifa wa  Allah  (s.w)  katika  ardhi,  yaani kuwa  wasimamishaji  wa  Ufalme  wa Allah(s.w)  katika  ardhi  (Dola  ya Kiislamu)  kwa  niaba  yake  pamoja  na  kuwa  yeye  mwenyewe  ni Muweza  wa  kuusimamisha  kwa  kusema:  “kuwa”  na  “ukawa”.

2. Ili  kuweza  kusimamisha  ukhalifa katika  ardhi  watu hawanabudi  kuwa  na  ujuzi  wa  kutosha  juu  ya  mazingira  ya  ardhi na  namna  ya  kukabiliana  nayo.

Nabii  Adam(a.s)  kufundishwa “majina  ya  vitu  vyote”  ni  kielelezo  kuwa  alifunzwa  fani  zote  za elimu  zinazohitajika  katika  kuendea  kila  kipengele  cha  maisha  ya binafsi  na  ya  jamii  ya  mwanaadamu  hapa  ardhini.  

Pamoja  na elimu  ya  vitu  mbali  mbali  (elimu  ya  mazingira),  Adam(a.s)  na  kizazi chake  waliahidiwa  kuletewa  mwongozo  kutoka  kwa  Allah(s.w) utakaowawezesha  kusimamisha  ukhalifa  na  kuvuna  matunda  yake ambayo  ni  kuishi  kwa  furaha  na  amani  na  kupata  radhi  za Allah(s.w)  hapa  duniani  na  huko  akhera  kama  tunavyojifunza katika  aya  zifuatazo:

قُلْنَا اهْبِطُوا مِنْهَا جَمِيعًا ۖ فَإِمَّا يَأْتِيَنَّكُمْ مِنِّي هُدًى فَمَنْ تَبِعَ هُدَايَ فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُون
 “Tukasema:    Shukeni  humo  nyote  (kutoka  peponi)  na  kama ukikufikieni  uwongozi  utokao  kwangu,  wale  watakaoufuata uwongozi  wangu  huo,  haitakuwa  khofu  juu  yao  wala hawatahuzunika.(2:38)

وَالَّذِينَ كَفَرُوا وَكَذَّبُوا بِآيَاتِنَا أُولَٰئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ ۖ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ
Lakini  wenye  kukufuru  na  kuyakadhibisha  maneno  yetu,  hao  ndio watakaokuwa  watu  wa  motoni,  humo  watakaa  milele”.   (2:39)

3. Kusimamisha  ukhalifa katika  ardhi  au  kusimamisha Uislamu  katika  jamii  ni  jambo  linalompandisha  mwanaadamu hadhi  na  daraja  mbele  ya  Allah(s.w)  kuliko  ile  hadhi  na  daraja  ya Malaika  mbele ya Allah(s.w).

Hili  linadhihirika  pale  Malaika walipoamrishwa  kumsujudia  Adam(a.s).

Sijda  ni  kitendo  cha heshima  ya  hali  ya  juu  kinachomstahiki Allah(s.w)  peke  yake,  lakini kama  ishara  ya  kuonesha  hadhi  ya  Khalifa  (Naibu)  wa  Allah(s.w), hapa  ardhini,  Allah(s.w)  aliwaamrisha  Malaika  wamsujudie  Adam na  wakatii.
Ubora  wa  kusimamisha  Ukhalifa  (Uislamu)  katika  jamii pia  unadhihirishwa  katika  aya  zifuatazo:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا هَلْ أَدُلُّكُمْ عَلَىٰ تِجَارَةٍ تُنْجِيكُمْ مِنْ عَذَابٍ أَلِيمٍ

“Enyi  mlioamini!    Je!    Nikujulisheni  biashara  itakayokuokoeni na  adhabu  iumizayo?(61:10)

(Biashara  yenyewe  ni  hii);-  
تُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ وَرَسُولِهِ وَتُجَاهِدُونَ فِي سَبِيلِ اللَّهِ بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ ۚ ذَٰلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُون
Muaminini  Mwenyezi  Mungu  na Mtume  wake  na  piganieni  Dini  ya  Mwenyezi  Mungu  kwa  mali zenu  na  nafsi  zenu,  haya  ni  bora kwenu  ikiwa  mnajua”.  (61:-11)

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA HISTORIA.

Ndugu wasomaji wa blog hii ya isspyetu baada ya kuangalia mtazamo wa wasiokuwa waislamu juu ya historia sasa tuangalie mtazamo wa waislamu juu ya historia





 by Ahmed Mnungamo



 Imeshabainishwa  kuwa  Historia,  kwa  ujumla,  ni  kumbukumbu za  matendo  na  matukio  yanayohusu  maisha  yote  ya  mwanaadamu katika  jamii  yake  kwa  muda  wote  uliopita

Uislamu  unaitizamaje  Historia  ya  mwanaadamu?

Mtizamo  wa Uislamu  juu  ya  historia  kwa  ujumla  unatofautiana  sana  na  ule  wa makafiri.

Ambapo  makafiri  wanadai  kuwa  hapana  Muumba  wa Ulimwengu  na  vyote  vilivyomo  kwa  ujumla,  Uislamu  unauhusisha Ulimwengu  (Universe)  na  vyote  vilivyomo  akiwemo  mwanaadamu, na  Muumba  mmoja  tu  Mwenye  Hekima  na  Ujuzi  usio  na  kikomo, ambaye  ameumba  kila  kitu  kwa  lengo  maalumu.

LENGO LA MAUMBILE YOTE YALIYOMZUNGUKA MWANADAMU.

Mwenyewe Muumba Allah(s.w),  anabainisha  lengo  la  kumbwa mbingu  na  ardhi  na  vyote  vilivyomo  katika  aya  zifuatazo:

MEAT CAKE (Keki ya nyama )



MEAT   CAKE
(Keki ya nyama )

VIFAA VYAKE
  1.  Nyama ya kusaga kilo moja na nusu
  2. Saigi robo kilo
  3. Unga wa ngano robo kilo
  4. Mayai 18
  5. Uzile vijiko viwili
  6. Baking powder vijiko viwili vya chai
  7. Ndimu moja , thomu kidogo , mdalasini na pilipili manga na pilipili boga kidogo
HATUA ZA UTENGENEZAJI
  1. Changanya  nyama ,pilipili,  manga, thomu, mdalasini na uzile na uvipike pamoja mpaka viive
  2. Saga  siagi na mayai sita hadi iwe cream na nyepesi kama keki ya sukari
  3. Changanya  pamoja na unga wa baking poweder changanya kwa mkono mpaka uchanganyike sawasawa
  4. Piga  mayai mengine sita uyachanganye na ile nyama kwa kijiko mpaka ichanganyike vizuri
  5.  Para  karoti kwa kibati cha kuparia chipsi nazo ziwe kama chipsi na uzichemshe mpaka ziwive
  6.   Kata  pilipili boga ziwe slice za duara
  7. Paka  siagi tray yako ya kuchomea ienee yote nzima na mimina ule mchanganyiko wa keki yako na utandaze juu yake ule mchanganyiko wa nyama na mayai
  8. Vunja  yale mayai sita yaliyo baki nayapige vizuri
  9. Tandaza  chipsi za karoti na zile  slice za pilipili mboga
  10. Nyunyiza  yale mayai hadi yaenee mote



  1. 11.  Tia  katika oven au pambia mpaka ikauke na iwive na ikisha poa tayari kwa kuliwa
Download pdf documents ya makala hiyo
 
 
 
 
 

MTIZAMO WA SAYANSI JUU YA CHANZO CHA ULIMWENGU NA UHAI.

by Ahmedi Mnungamo

Sayansi  ya  leo  hutufunza  kuwa  dunia,  nyota  na  sayari  zote zina  umri  maalum  na  kwamba  zimetokea  katika  kipindi  Fulani  cha wakati. 

Hata  hivyo  ni  vigumu  mno  kwa  sayansi  kutoa  kipindi  hakika (tarehe/siku)  ulimwengu  ulipoanza  kutokea. 

Baadhi  ya wanasayansi  hukisia  kuwa  ulimwengu  huu  umetokea  kiasi  cha miaka  kati  ya  15  hadi  20  bilioni  iliyopita.

Wanasayansi  hutuambia  kuwa  ulimwengu  mwanzoni  kabisa umetokana  (au  umetengenezwa)  na  hewa  au  moshi  (a  gaseous mass)  ambayo  inakisiwa  hasa  kuwa  ni  hydrogen. 

Hatimaye  bonge hilo  la  hydrogen  lilitenganishwa  na  kufanya  vipande  vidogo  vidogo ambavyo  vilifanya  galaxies. 

Galaxy  yetu  yakisiwa  kutokea  miaka kama  bilioni  kumi  iliyopita.

 Vipande  vipande  vilivyofanya  galaxy ndivyo  hivyo  vilivyounda  Solay  System  kwa  kuchangukana  zaidi (fragmentation). 

Bonge  la  mwanzo  la  hewa  (gaseous  mass) laweza  kuwa  limetokea  kwa  njia  ya  mshindilio  ‘(condensation)’.