IJUWE SWALA YA MAITI NA NAMNA YA KUISWALI
Kumswalia Maiti.
·
Masharti
ya Swala ya Maiti.
- Kwa wenye
kumswalia maiti, watekeleze masharti ya kawaida ya swala.
- Masharti
ya maiti anayeswaliwa:
o
Maiti awe muislamu
o
Maiti iwe imeoshwa na kukafiniwa
o
Maiti iwekwe mbele ya wanaoisalia.
-- Inajuzu kusalia maiti iliyo masafa ya mbali
(swala ya ghaibu).
-- Maiti zikiwa nyingi zipangwe
mbele, za kiume zikiwa karibu
na imamu kisha kusaliwa zote kwa pamoja.
na imamu kisha kusaliwa zote kwa pamoja.
o
Maiti isiwe ya shihidi.
-- Kwa
mujibu ya Hadith ya Mtume (s.a.w), mashahidi hawaoshwi wala kusaliwa.
·
Nguzo za
Swala ya maiti.
- Swala ya maiti
inaswaliwa wima; haina rukuu, sijda wala kikao.
- Nguzo
za swala ya maiti ni;
i.
Nia
ii.
Takbira ya kuhirimia
iii.
Kusoma Suratul-Faatiha.
iv.
Takbira ya Pili.
v.
Kumswalia Mtume (s.a.w) kama
tufanyavyo kwenye Tahiyyatu.
vi.
Takbira ya Tatu.
vii.
Kumuombea dua maiti.
viii.
Takbira ya Nne.
ix.
Kuombea dua waislamu wote, kisha kutoa Salaam.
·
Namna ya
kutekeleza swala ya Maiti hatua kwa hatua.
Utaratibu wa kusimamisha swala ya maiti ni kama ifuatavyo;
a)
Maiti iwekwe mbele.
b) Imamu asimame katikati ya mwili wa maiti ikiwa maiti ni
ya kike, na usawa wa mabega kama maiti ni ya
kiume.
c)
Maamuma watasimama kwenye mistari (safu) kwa idadi ya
witiri; 1, 3, 5, n.k.
d)
Baada ya hapo swala itaanza na kuendelea kama ifuatavyo:
i.
Nia - ambayo ni kukusudia moyoni.
ii.
Kuleta takbira ya kwanza; kwa kusema, “Allaah Akbar”
iii.
Imamu na maamuma watasoma suratul-Faatiha – kimya kimya.
iv.
Imamu ataleta Takbira ya Pili kisha maamuma – kimya
kimya kwa maamuma na si lazima kuinua mikono wao.
v.
Kumswalia Mtume (s.a.w) kama
ilivyo katika Tahiyyatu, wote – kimya kimya.
vi.
Imamu ataleta takbira ya Tatu kisha maamuma- kama walivyofanya awali.
vii. Wote kumuombea maiti dua kimya kimya, ikiwemo:“Allaahumma ghfirlihayyinaawamaayyitinaa washaahidinaa waghaaibinaa waswaaghirinaa wakaabirinaa
wadhakirna waunthaanaa. Allaahumma manahyaytahuuminnaa faahyi ‘alal Islaam.
Waman tawaffaytahuu minnaa tawaffahuu ‘alal Imaani. Allaahumma laa tahirimnaa
ajirahuu walaa taftinaaba’adahuu”
Tafsiri:
“Ewe Allah tusamehe
sisi, na maiti wetu, na mashahidi, na wasiokuwepo miongoni wetu, vijana wadogo
miongoni mwetu na wakubwa miongoni mwetu, wanamume wetu, na wanawake wetu. Ewe
Allah, yeyote yule miongoni mwetu utakayemewezesha kuishi, mjaalie aishi katika
Kiislamu na yeyote miongoni mwetu utakayemfisha, mfishe katika Imani (ya
Kiislamu). Ewe Allah, usitukatishe ujira kutoka kwake na wala usitufitinishe
baada yake.”
- Au kwa kifupi tuweza kumuombea maiti kama ifuatavyo;
“Allaahumma ghfir lahuu warhamhuu wa-afihii
wa-afu-anhu”
Tafsiri:
“Ewe Allah, Mghufirilie na
Umrehemu”.
viii.
Imamu ataleta Takbira ya nne na maamuma kufuatihia kama awali.
ix.
Wote watawaombea waislamu dua – (pia si lazima kuleta
dua hii).
Rejea Qur’an (59:10).
x.
Imamu kutoa salaam na maamuma kufuatishia bila kutoa
sauti kama ilivyo kwenye swala ya kawaida kwa
kusema;
“Assalaamu ‘alaykum
Warahmatullaah (Wabarakaatuh)”
Tafsiri:
“Amani
iwe juu yenu na Rehema za Allah na Baraka zake”.
No comments:
Post a Comment