Umuhimu Wa Kukimbilia Kutekeleza Nguzo Ya Hajj
Anasema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
إِنَّ أَوَّلَ بَيْتٍ وُضِعَ لِلنَّاسِ لَلَّذِي بِبَكَّةَ مُبَارَكًا وَهُدًى لِّلْعَالَمِينَ ﴿٩٦﴾
96. Hakika nyumba ya awali iliyowekwa kwa
ajili ya watu (kufanya ‘ibaadah) ni ile ambayo iko Bakkah (Makkah),
yenye barakah na mwongozo kwa walimwengu.
فِيهِ
آيَاتٌ بَيِّنَاتٌ مَّقَامُ إِبْرَاهِيمَ ۖ وَمَن دَخَلَهُ كَانَ آمِنًا ۗ
وَلِلَّـهِ عَلَى النَّاسِ حِجُّ الْبَيْتِ مَنِ اسْتَطَاعَ إِلَيْهِ
سَبِيلًا ۚ وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ ﴿٩٧﴾
97. Ndani yake kuna Aayaat (ishara, dalili)
zilizo wazi; mahali pa kisimamo cha Ibraahiym. Na mwenye kuingia humo
anakuwa katika amani. Na kwa ajili ya Allaah ni wajibu kwa watu
watekeleze Hajj katika Nyumba hiyo kwa mwenye uwezo. Na atakayekufuru,
basi hakika Allaah ni Mkwasi kwa walimwengu. [Aal-‘Imraan 96-97]Na kauli ya Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
عن
أبي عَبْدِ الرَّحْمنِ عَبْدِ اللهِ بنِ عُمَرَ بنِ الخَطابِ رَضيَ اللهُ
عنهُما قال: سَمِعْتُ رسُولَ الله صلى الله عليه وسلم يقولُ: ((بُنَي
الإسلامُ على خَمْسٍ: شهادَةِ أَنْ لا إلهَ إلا اللهُ وأَنَّ محمَّداً
رسولُ اللهِ، وإقَامِ الصَّلاةِ، وإيتَاءِ الزَّكاةِ، وحَجِّ البَيْتِ،
وصَوْمِ رَمَضَانَ )) رَوَاهُ الْبُخَارِيُّ
Kutoka
kwa Abuu 'Abdir-Rahmaan 'Abdullaah bin 'Umar bin
Al-Khattwaab (Radhwiya Allaahu 'anhumaa) amesema: Nimemsikia Rasuli wa
Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema: “Uislamu
umejengwa kwa nguzo tano: Kukiri na kushuhudia kwamba hapana Muabudiwa
wa haki isipokuwa Allaah na Muhammad ni Rasuli Wake, kusimamisha
Swalaah, kutoa Zakaah na kuhiji Al-Bayt (Makkah) na kufunga swawm
Ramadhwaan.” [Al-Bukhaariy na Muslim]Tunatambua kutokana na kauli hizo kuwa kutekeleza Hajj ni fardhi kwa kila mwenye uwezo. Hivyo asiyeharakisha kutekeleza fardh hii atakuwa amemuasi Rabb wake na Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na itakuwa ni dhambi kubwa kwake ikiwa kuacha huko ni kwa makusudi na hali alikuwa ana uwezo wa mali, siha n.k., sababu atakuwa amekanusha amri ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa): more>>
وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ مَّاذَا تَكْسِبُ غَدًا ۖ وَمَا تَدْرِي نَفْسٌ بِأَيِّ أَرْضٍ تَمُوتُ ۚ إِنَّ اللَّـهَ عَلِيمٌ خَبِيرٌ ﴿٣٤﴾
Na nafsi yoyote haijui nini itachuma kesho, na nafsi yoyote haijui itafia katika ardhi gani, hakika Allaah ni Mjuzi wa yote, Mwenye upeo wa khabari za dhahiri na za kufichika. [Luqmaan: 34].
b-Wengine wameshughulika na anasa za dunia na kughafilika kuwa huenda wakaaga dunia na kukosa kutekeleza nguzo hii ya Uislamu. Tambua ndugu unayechelea kutekeleza Hajj kwamba nafsi inayojidhulumu hujuta wakati wa kutolewa roho na mtu hutamani arudi atende yale aliyoyakosa kutenda lakini haiwezekani tena kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
حَتَّىٰ إِذَا جَاءَ أَحَدَهُمُ الْمَوْتُ قَالَ رَبِّ ارْجِعُونِ ﴿٩٩﴾
Mpaka itakapomfikia mmoja wao mauti, atasema: “Rabb wangu! Nirejeshe (duniani).”
لَعَلِّي
أَعْمَلُ صَالِحًا فِيمَا تَرَكْتُ ۚ كَلَّا ۚ إِنَّهَا كَلِمَةٌ هُوَ
قَائِلُهَا ۖ وَمِن وَرَائِهِم بَرْزَخٌ إِلَىٰ يَوْمِ يُبْعَثُونَ ﴿١٠٠﴾
“Ili nikatende mema katika yale
niliyoyaacha.” (Ataambiwa) “Laa hasha!” Hakika hilo ni neno alisemaye
yeye tu. Na nyuma yao kuna barzakh mpaka Siku watakayofufuliwa. [Al-Muuminuwn: 99-100].3-Hajj Ni Katika ‘Amali Bora Kabisa
عَنْ
أَبِي هُرَيْرَةَ أَنَّ رَسُولَ اللَّهِ صَلَّى اللَّهم عَلَيْهِ
وَسَلَّمَ سُئِلَ أَيُّ الْعَمَلِ أَفْضَلُ فَقَالَ: ((إِيمَانٌ بِاللَّهِ
وَرَسُولِهِ)) قِيلَ ثُمَّ مَاذَا قَالَ: ((الْجِهَادُ فِي سَبِيلِ
اللَّهِ)) قِيلَ ثُمَّ مَاذَا قَالَ: ((حَجٌّ مَبْرُورٌ)) متفق عليه
Aliulizwa
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) Ipi
'amali njema kabisa? Akasema: ((Kumuamini Allaah na Rasuli Wake))
Akaulizwa: "Kisha nini"? Akasema: ((Jihaad katika Njia ya Allaah))
Akaulizwa: "Kisha nini"? Aakasema: ((Hajj yenye kukubaliwa)). [Al-Bukhaariy na Muslim].4-Mwenye Kutekeleza Hajj Hufutiwa Madhambi Yote
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) قَالَ: سَمِعْتُ النَّبِيَّ (صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) يَقُولُ: ((مَنْ حَجَّ لِلَّهِ فَلَمْ يَرْفُثْ وَلَمْ يَفْسُقْ رَجَعَ كَيَوْمِ وَلَدَتْهُ أُمُّهُ)) متفق عليه
Kutoka
kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) ambaye amesema: Nimemsikia
Rasuli wa Allaah (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) akisema:
((Atakayefanya Hajj, kisha asiseme maneno machafu wala asitende vitendo
vichafu atarudi akiwa kama siku aliyozaliwa na mama yake)) [Al-Bukhaariy na Muslim].5-Jazaa Ya Kutekeleza Hajj Ni Kuingizwa Jannah
عَنْ أَبِي هُرَيْرَةَ (رضي الله عنه) أَنَّ رَسُولَ اللهِ (صَلَّى اللهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ) قَالَ: ((العُمْرَةُ إِلَى العُمْرَةِ كَفَّارَةٌ لِمَا بَيْنَهُمَا، وَالحَجُّ المَبْرُورُ لَيْسَ لَهُ جَزَاءٌ إِلَّا الجَنَّةَ)) متفق عليه
Kutoka
kwa Abuu Hurayrah (Radhwiya Allaahu 'anhu) kwamba Rasuli wa Allaah
(Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: (('Umrah hadi
'Umrah ni kafara (kufutiwa dhambi) baina yao, na Hajjul-Mabruwr [yenye
kukubaliwa] haina jazaa isipokuwa ni Jannah)) [Al-Bukhaariy na Muslim].Tafadhali bonyeza kiungo kifuatacho upate faida tele nyinginezo:
Fadhila Za ‘Umrah Na Hajj - Kutoka Kitabu: Alhidaaya Katika Manaasik Za Hajj Na 'Umrah
Tunamuomba Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa) Awajaalie Waislamu ambao bado hawakujaaliwa kuitekeleza fardhi hii, uwezo wa kutekeleza Hajj na Awaghufurie madhambi yao na Awathibitishe katika Manhaj ya Salaf mpaka mwisho wa uhai wao. Aamiyn.
mada imekuja wakati muafaka
ReplyDelete