by Ahmedi Mnungamo
Sayansi ya leo hutufunza kuwa dunia, nyota na sayari zote zina umri maalum na kwamba zimetokea katika kipindi Fulani cha wakati.
Hata hivyo ni vigumu mno kwa sayansi kutoa kipindi hakika (tarehe/siku) ulimwengu ulipoanza kutokea.
Baadhi ya wanasayansi hukisia kuwa ulimwengu huu umetokea kiasi cha miaka kati ya 15 hadi 20 bilioni iliyopita.
Wanasayansi hutuambia kuwa ulimwengu mwanzoni kabisa umetokana (au umetengenezwa) na hewa au moshi (a gaseous mass) ambayo inakisiwa hasa kuwa ni hydrogen.
Hatimaye bonge hilo la hydrogen lilitenganishwa na kufanya vipande vidogo vidogo ambavyo vilifanya galaxies.
Galaxy yetu yakisiwa kutokea miaka kama bilioni kumi iliyopita.
Vipande vipande vilivyofanya galaxy ndivyo hivyo vilivyounda Solay System kwa kuchangukana zaidi (fragmentation).
Bonge la mwanzo la hewa (gaseous mass) laweza kuwa limetokea kwa njia ya mshindilio ‘(condensation)’.
Kwa njia hii hydrogen ilitoa helium, kisha Carbon na Oxygen kwa hivyo kukatokea madini ya kila namna.
Kuhusu chanzo cha uhai sayansi hutufahamisha kuwa uhai umeanzia majini na kwamba maji hufanya sehemu kubwa ya chembe hai zote.
Viumbe wa mwanzo walikuwa ni wenye chembe hai moja – “Unicellular Organisms” na hivyo walikuwa ni wadogo mno kiasi cha kutokuweza kuonekana na macho ya kawaida (mpaka darubini yenye nguvu sana).
Hata hivyo sayansi yatuonyesha kuwa chembe moja (Cell) hiyo ya viumbe hao ilikuwa ina kila kitu ambacho kilihitajika kwa uhai.
Palikuwa na “Cytoplasm”, “Nucleus”. “Chromosomes” zenye “genes” na kila chenye kuufanya uhai uwepo.
Viumbe hawa wenye chembe hai moja kama “amoeba” wapo hadi hii leo.
Na kama tulivyotangulia kutaja wanasayansi hudhani hivi ndivyo viumbe vya mwanzo kutokea.
Maelezo haya ya wanasayansi hutupa picha ni wapi uhai ulianzia na viumbe gani wa mwanzo kutokea.
Lakini hayatupi
Maelezo ni vipi uhai huu wenye utata (complex) kiasi hicho ulitokea.
Akishangaa kuhusu utata wa uhai na chanzo chake, Dr. Mourice Bucaille ana haya ya kusema:
As far as I am concerned, however, the brilliant analysis of the way this system works (for each and every cell is a kind of computer comprised of innumerable interrelations) is just as amazing as the general conclusions cited above concerning the supposed resolution of unexplained facts on the origins of life.
One very important question of these investigations: How could a system as complex as this have been formed? Was it the work of chance, following a host of trials and errors? That seems most unlikely. What other logical theories are there? It is common knowledge that a computer will only function if it has been programmed, a fact that implies the existence of a programming intellect, that provides the information required to operate the system. That is the problem facing all thinking people who refuse to accept mere words or groundless theories, people who will only acknowledge conclusions based on facts. Given the present state of knowledge, however, science has not provided any answer to this precise point.
Tafsiri:
Kwa namna ninavyoona mimi, kwa jinsi mfumo huu (wa maisha) unavyofanya kazi (kila chembe hai ni kama namna ya kompyuta iliyofanyika kwa ushirikiano na maingiliano ya vitu chungu nzima) ni jambo la kustaajabisha unapoangalia ukweli wa chanzo cha uahi. Suala moja ambalo linafungamana na uchunguzi huu ni kwamba, ni vipi mfumo huu (system) ulio tata (complex) umeweza kuundwa? Je! Ilitokezea kwa bahati nasibu baada ya majaribio? Hii haingii akilini. Kuna ufafanuzi wowote ule? Inabainika wazi kuwa kompyuta haiwezi kufanya kazi bila ya kupangiliwa vyema (programmed), unaobainisha kuwepo kwa mpangaji mweledi anayetoa habari zinazohitajika
katika kuuendesha mfumo huo. Hilo ndilo tatizo linalowakumba watu wenye kutumia akili zao ambao hutaka kujua ufafanuzi wa masuala, watu wanaokataa kukubali maneno matupu yasio na ithibati au nadharia zisizo na utegemezi wowote, watu watakaokubaliana na maelezo yaliyofungamana na kweli tupu. Hata hivyo hadi hivi sasa, sayansi haijatoa jibu lolote lile lililo sahihi.
Maelezo haya ya mwanasayansi Dr. Bucaille yanatosha kututhibitishia kuwa sayansi haina jibu kamili na sahihi juu ya chanzo cha uhai.
Sayansi Yasemaje
Kuhusu Dhana Kuwa Mwanadamu Katokana na Kizazi cha Manyani.
Wanahistoria wa Kikafiri hudai kuwa mwanaadamu ametokana na kizazi cha manyani kama tulivyoona kaitka kurasa za nyuma.
Wao huinasibisha dhana yao hiyo na sayansi.
Madai hayo ni uwongo; kwani sayansi haikubaliani kabisa na dhana hiyo.
Hapa tunapenda tumnukuu tena mwanasayansi mashuhuri Dr. Maurice Bucaille (Surgeon) akitoa maelezo juu ya chanzo cha mwanadamu:
There is absolutely no scientific proof to suggest that man was born of the evolved forms of present-day apes. On the contrary, everything argues against this outmoded theory. What science has shown is that, at a certain point in time, a human species appeared which gradually transformed itself into today’s man. From a scientific point of ivew, the crux of problem is that we do not know what man evolved from: Was it from an autonomous lineage or from one that could be connected with another animal lineage? Science does not supply indisputable indication as to the actual moment that the transformation took place; nor on the initial matter employed in the process: Many of the ways in which the change occured remain a mystery to us.
Tafsiri:
Hakuna ushahidi wowote wa kisayansi unaosema kuwa binaadamu alitokana na nyani hawa wa siku hizi.
Kinyume chake ni kuwa nadharia hii ya kale inapingwa.
Sayansi imeonyesha kuwa katika wakati fulani, binaadamu alianza kukua kidogo kidogo (hatua kwa hatua) mpaka kufikia hii hatua aliyo leo.
Katika mtazamo wa kisayansi, ugumu wa tatizo uko kwenye suala la binaadamu alitokana na nini? Je, ilikuwa kutokana na uzao usiojulikana au uzao ambao unaweza kuhusishwa na wanyama.
Sayansi haitoi dalili zisizopingika (zisizo na mushkeli) zinazoeleza ni lini chanzo cha binaadamu kilianza, wala dalili zinazoonyesha kitu cha mwanzo kinachohusika na chanzo hicho. Ni kusema kuwa njia nyingi zinazoonyesha namna mabadiliko yalivyotokea, hatuwezi kuzielezea.
Hatuhitaji kutoa maelezo zaidi kuweka wazi kuwa mwnaadamu hatokani na nyani, kwani maelezo haya ya Dr. Bucaille yapo wazi kabisa.
Neno la kusisitiza hapa tu ni kuwa, maelezo mengi yaliyo kwenye vitabu vya historia kuwa binaadamu katokana na kizazi cha manyani si maelezo ya kisayansi. Bali makafiri huisingizia sayansi ili wapate kuustawisha ukafiri wao.
Nimemaliza mtazamo wa makafiri juu ya historia