MEAT CAKE (Keki ya nyama )



MEAT   CAKE
(Keki ya nyama )

VIFAA VYAKE
  1.  Nyama ya kusaga kilo moja na nusu
  2. Saigi robo kilo
  3. Unga wa ngano robo kilo
  4. Mayai 18
  5. Uzile vijiko viwili
  6. Baking powder vijiko viwili vya chai
  7. Ndimu moja , thomu kidogo , mdalasini na pilipili manga na pilipili boga kidogo
HATUA ZA UTENGENEZAJI
  1. Changanya  nyama ,pilipili,  manga, thomu, mdalasini na uzile na uvipike pamoja mpaka viive
  2. Saga  siagi na mayai sita hadi iwe cream na nyepesi kama keki ya sukari
  3. Changanya  pamoja na unga wa baking poweder changanya kwa mkono mpaka uchanganyike sawasawa
  4. Piga  mayai mengine sita uyachanganye na ile nyama kwa kijiko mpaka ichanganyike vizuri
  5.  Para  karoti kwa kibati cha kuparia chipsi nazo ziwe kama chipsi na uzichemshe mpaka ziwive
  6.   Kata  pilipili boga ziwe slice za duara
  7. Paka  siagi tray yako ya kuchomea ienee yote nzima na mimina ule mchanganyiko wa keki yako na utandaze juu yake ule mchanganyiko wa nyama na mayai
  8. Vunja  yale mayai sita yaliyo baki nayapige vizuri
  9. Tandaza  chipsi za karoti na zile  slice za pilipili mboga
  10. Nyunyiza  yale mayai hadi yaenee mote



  1. 11.  Tia  katika oven au pambia mpaka ikauke na iwive na ikisha poa tayari kwa kuliwa
Download pdf documents ya makala hiyo
 
 
 
 
 

1 comment:

  1. karibuni wadau mtoe maoni yenu na maswali pia mwaweza uliza

    ReplyDelete