MEAT CAKE
(Keki ya nyama )
VIFAA VYAKE
- Nyama ya kusaga kilo moja na nusu
- Saigi robo kilo
- Unga wa ngano robo kilo
- Mayai 18
- Uzile vijiko viwili
- Baking powder vijiko viwili vya chai
- Ndimu moja , thomu kidogo , mdalasini na pilipili manga na pilipili boga kidogo
HATUA ZA UTENGENEZAJI
- Changanya nyama ,pilipili, manga, thomu, mdalasini na uzile na uvipike pamoja mpaka viive
- Saga siagi na mayai sita hadi iwe cream na nyepesi kama keki ya sukari
- Changanya pamoja na unga wa baking poweder changanya kwa mkono mpaka uchanganyike sawasawa
- Piga mayai mengine sita uyachanganye na ile nyama kwa kijiko mpaka ichanganyike vizuri
- Para karoti kwa kibati cha kuparia chipsi nazo ziwe kama chipsi na uzichemshe mpaka ziwive
- Kata pilipili boga ziwe slice za duara
- Paka siagi tray yako ya kuchomea ienee yote nzima na mimina ule mchanganyiko wa keki yako na utandaze juu yake ule mchanganyiko wa nyama na mayai
- Vunja yale mayai sita yaliyo baki nayapige vizuri
- Tandaza chipsi za karoti na zile slice za pilipili mboga
- Nyunyiza yale mayai hadi yaenee mote
- 11. Tia katika oven au pambia mpaka ikauke na iwive na ikisha poa tayari kwa kuliwa
karibuni wadau mtoe maoni yenu na maswali pia mwaweza uliza
ReplyDelete